Monday, February 11, 2008

Love Love Love

Je, bila upendo unaweza kuishi? Bila shika kila mmoja wetu anajibu tofati kadiri ya tafsiri ya neno Love au Upendo lilivyo. Basi niwape nafasi kutafuta ukweli upo wapi.

How would you respond to someone who comes infont of you and says I L O VE you?

It is very simple to answer this Question Just say to her, Thank You, I LOVE you too. You guys don't think too much, you will loose more Kilokarolies while the Lady just ment to say she loves you the way you are.

Look down what do you see!
That is Love. We were Created by God to Love each other, do you do the same or you are looking for something else?



Mpendwa msomaji wangu, mmoja alipata kigugumizi kidogo akaamua kuniuliza moja kwa moja, kwamba anashindwa kufikia uamuzi wake wa kutaka kuishi na mwandani wake, kwa kuwa mwili moja.

Na mimi nilimshukuru kwa kufikia uamuzi huu, kwani mara nyingi tumeingia pupa katika fani na hatimaye tunajikuta tunaangukia pua. Naomba uambatane nami katika kuyachambua haya machache :-

Mambo mhimu ya kuzingatia

  • Mchague mtu ambaye unauhuru wa kuongea naye
Wengi wamekuwa wakipotea njia na kuchagua watu ambao sio matamanio yao wala hawafurahii kuongea nao, kuongea ni sanaa ambayo inahitaji ufundi na ujuzi kama fani zingine katika kupanga maneno na kupendezesha au kunogesha mazungumzo. Matokeo yake wakisha kaa kama mme na mke, mme anaamua kurudi nyumbani kwa kuchelewa akisingizia kazi nyingi. Lakini ukweli ni kwamba nyumba imeingi Luba, hakuna maongezi ya kunogesha upendo wenu.
  • Mchague mtu mnayeendana kitabia au walau kulandana katika mambo fulani
Hii itakupa furaha kwani muda mwingi ambao mtakuwa pamoja utapenda kusikia mawazo yake na kusikia kipya toka kwake. Na hii itadumisha upendo baina yenu.
  • Uwe sababu ya yeye kuwa na furaha
Hapa nataka kumanisha kuwa naomba uepukane na vitu ambavyo vitakuwa hatarishi kwa uhusiano wenu.
Kwa mfano: kuwa chagua marafiki wenye tabia zuri, kutawafanya muwe na furaha kwani kesi za mara kwa mara na marafiki zenu hazitakuwepo.

-Hakutakuwa na kuingiliana Nyumba

-Hakutakuwa na masengenyano yasiyo na vichwa wala miguu

-Hakutakuwa na kuchuguzana leo jirani anakula mboga gani au amevaa nguo ya aina gani
  • Muwe watu wa furaha
Utashangaa kuona watu wanaishi nyumba moja ila wanajifunika shuka tofauti, hasa kwa nini kuusemea moyo? Hujui kwamba huyo ndiyo wako mpaka mauti yatakapo watenga, na kama leo unafanya hivi, si unampa jibu kwamba nenda kungine kwangu ulipotea njia?
  • Shirikishaneni matatizo yanayowapata katika maisha
Ukifanya hivi kila mmoja atamjali mwenzake kwani hakutakuwa na kutiliana mashaka katika uhusiano wenu.
  • Pakitokea mtafaruku wa mawasiliano baina yenu kaeni chini muongelee tofauti zenu
Kuzungumzia tofauti baina yenu kutawafanya mjenge mahusiano mazuri na ya kuaminiana, naomba nikuulize swali, wangapi leo wanakaa na wake zao au waume zao na kuwauliza kwa upole juu ya mapungufu waliyoyasikia? Na unachukua uamuzi gani baada ya kusikia hayo kutoka kwa mwenzi wako?
  • Usipende kuamini kila unaloambiwa na watu juu ya yule unayempenda, au mwenzi wako
Tumia muda mwingi kumsoma mpendwa wako kabla hujafikia uamuzi wa kumfanya awe mwenzi wako. Ni nafasi mhimu sana kufahamiana, bila hilo migongano mingi itajitokeza. Na sababu yake ni kwamba hukuwa makini mwanzoni wakati unafanya uamzi wako.

Jaribu kuutafuta ukweli wa jambo kabla ya kufikia maamuzi, jambo ambalo umekusudia kulitekeleza.


  • Usimtendee mwenza wako jambo ambalo wewe usingependa kutendewa
Kitu kinginne cha msingi hapa ninachotaka wote kutambua ni kwamba, usimtendee mwenza wako (mke wako) jambo ambalo wewe usingependa kutendewa. Na ikiwa limetukia kwa ajali, binadamu ndiye binadamu, basi ni vema kumwomba radhi mwenza wako tena kwa adabu. Kumbuka kwamba haya hayapatikani kwa kila mtu ila kwa wanaume wachache wanaomjua Mungu, na si tu kumjua Mungu bali pia awe ni mtu anayejishughulisha na mambo ya Kanisa hii itakuwa kama chachu ya yeye kukuza uhusiano wake na Mungu na wako pia.

Mwisho Maandiko Matakatifu yatufundisha jinsi ilivyo vema kwa ndugu kuishi kwa moyo moja na roho moja. Kutatupunguzia magonjwa ya moyo, ambayo tunakutana nayo katika maisha.

No comments: