Saturday, February 16, 2008

Baraza la Mawaziri Tanzania

Hii ni Kasi Mpya Ari Mpya na Nguvu Mpya


Naufurahia msemo huu kwani kasi mpya haiwi tu kwa maneno lazima iwe pia kwa vitendo ili iwezekuthibitika. Nguvu mpya lazima mtu ajue kuvumilia magumu na halafu anaibuka na nguvu mpya katika kukabiliana na jambo lingine, Ari mpya inatukumbusha kutokata matumaini, kila kitu kinauvumbuzi hakuna tatizo lisilo na mwanzo wake, na hakuna Hesabu isiyo na Jibu, vile vile ukizaliwa kumbuka kwamba kunakufa. Ikiwa ulisifiwa kataka jambo furani kumbuka kutunza heshima ya sifa uliyopewa, ukijisahau yatakukuta haya mabadiliko yasiyokusudiwa. Lakini ili tusonge mbele hatuna budi kutolea sadaka walio makafara.

Mimi naongea na Mh. Jk na kumwuliza maswali kadhaa na yeye anajibu kama ifuatavyo:-

Mwadishi. Mbona sura nyingine sizioni?
Jk. Wameomba kupumzika!
Mwandishi. Mbona wengine wanalia kama wameomba kupumzika kwa hiari?
Jk. Hao wanaolia wanayao!
Mwandishi. Umeamua kumwaga na rafiki yako wa damu?
Jk. Alikuwa anajibu kuchezea shilingi chooni alifikiri haitatumbukia, umeona mwenyewe kilichofanyika!!
Mwandishi. Yaani ndo kusema umeamua kufanya kweli mzee?
Jk. Ili maandiko ya timie haina budi wengine kutolewa kafara, na mimi nimetolea kafara kondoo wangu, ili mjue kuwa ninauchungu na Ninyi Watanzania.
Mwandishi. Mimi nilifikiri unatania kumbe kweli?
Jk. Ulisha wahi kukamata kisu kwenye makali harafu usikatwe, au unategemea nini kama unachezea moto?

Mwndishi. Mzee tutakufa njaa ?
Jk.
Kama uligundua kwamba utakufa njaa ungefanya kazi kwa bidii na maarifa ili uwe na uhakika wa kupata Unga wa kesho. Kumbuka njia ya mkato ni nzuri na ina hasara zake, sasa unalilia nini, haya yaliyotukia uliyataka mwenyewe kwani hukujua kama unaiba?
Mwandishi. Mimi nilikuwa najaribu tu nione kama utagundua ...... nani ....
Jk. Sijazaliwa leo kwa heri ......
Mwandishi. Amaa kweli nilitegemea nitafichwa na wenzangu kumbe ndiyo wamenianika sasa mimi nitakuwa mgeni wa nani?


Baraza la Mawaziri


No comments: