Sunday, February 3, 2008

Je, kumshukuru Mungu ni jambo la lazima au la hiari?

Mpendwa, nimeweka swali hapo juu kwa makusudi mazima ili tuweze kuingia ndani ya mioyo yetu na kujichunguza, kwa kina kama kumshukuru Mungu ni jambo la hiari au unawajibika kumshukuru.

Kwa mimi binafsi nimejionea mambo mengi ambayo kwa mimi peke yangu bila uwezo wake mola nisingeliweza kuyatekeleza, hivyo basi nikatafakari kwa kina na nikatoa uamuzi wangu kuwa kwangu mimi kumshukuru Mungu kwa kila dakika ninayopewa ni wajibu. Ameniokoa katika mambo mengi na bado anaendelea kunilinda, sasa kwa nini nisimshukuru, na tena hajaniokoa tu bali amenisaidia wakati wa shida kujua njia ya kupita.

Nikusimulie yaliyonikuta kwenye mtihani, nilikuwa sijui kabisa baadhi ya maswali na mwalimu aliruhusu kumwuliza pale ambapo unahisi kunatautata katika kuelewa swali. Wenzangu waliuliza akawaelekeza na mimi nilipomwuliza akasema haelewi, kile nilicho mwuliza lakini haikuwa kweli kwamba haelewi alikuwa anafahamu lakini hakutaka kuniambia basi katika muda kama huu ndiyo unapojua kwamba miujiza ya Mungu inafanya kazi, mimi nilijibu vile nilivyo hisi kwamba linaweza kuwa jibu sahihi, ni kweli nilipata majibu ambayo mimi mwenyewe kwa uwezo wangu sikuya jua kabisa.

Ndipo nilipoamini kwamba Mungu hana hiana kwa wale wanaomwamini. Wewe mwenzangu je! Na wengi wetu tunakuwa na imani na Mungu hasa wakati tunapokabiliwa na shida kama mitihani, tunategemea kwamba Mungu afanye miujiza ili tufaulu, na wengine wetu ndo hawa somi kabisa wanategemea miujiza ya Mama Bikira Maria, katika dakika hizi za mwisho, na kwamba huko nyuma wala hawa kuwa wanajishughulisha naye kabisa.

Ndugu yangu huko ni kutaka kumkamua Mungu na Mama yetu Bikira Maria miujiza, kumbe busara ya kweli ni hii ya kujisaidia nami nitakusaidia, soma nami nitakusaidia pale ambapo umeshindwa kabisa.

Mshukuru Mungu kwa kukupa Afya njema

Tunakila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kutujalia zawaidi ya kuwa na afya njema, na hata uzuri tulionao, kama hufanyi hilo unamkosea haki Mungu wako aliyekuumba, na kutaka kuthibitisha kwamba unahaki ya kumshukuru basi jionee mwenyewe picha hapo chini.

Nami nakuuliza swali je hawa walisitahili kupata haya, bila shaka jibu ni hapana, je kwa nini sisi tusimshukuru kwa zawaidi ya uhai tuliojaliwa?



www.FunAndFunOnly.net (SridhaR)


www.FunAndFunOnly.net (SridhaR)


www.FunAndFunOnly.net (SridhaR)


www.FunAndFunOnly.net (SridhaR)


www.FunAndFunOnly.net (SridhaR)


www.FunAndFunOnly.net (SridhaR)


www.FunAndFunOnly.net (SridhaR)







No comments: