Saturday, January 26, 2008

Wema na ubaya wa mtu

Kwa kawaida kila mtu anawema wake na ubaya wake. Kwani tunaamini kwamba hakuna aliyemkamilifu kwa kila jambo.

Viongozi wanatumia vigezo vipi wanapotoa hukumu juu ya mtu kuwa huyu hatufai kuwa katika ushirika nasi? Hili limekuwa swali kubwa kwangu kwani wapo ambao tumewapoteza si kwa sababu hawafai kuwa kwa mfano watawa, mapadri, walimu, madaktari, au kuwa watu wenyewadhifa fulani katika jamii, ila kwa sababu ya tofauti za kawaida kati yake na kiongozi wake, anajikuta anaipoteza nafasi aliyoitegemea katika jamii.

Narudi kwenye swali langu, kwamba hawa viongozi wanaochukua dhamana ya maisha ya hawa watu, je, wanatumia vigezo vipi kutoa hukumu juu yao?

Dondoo nilizoziona kuwa zinakuwa kigezo cha mtu kutumia kumhukumu mwingine


Kijana kuonekana akimbishia mlezi wake, hata katika uhalisia wa jambo
Wapo waliofukuzwa kwa kuwa tofauti na walezi wao kwa kuwa hawakubaliani na mawazo yao katika kulelewa.

Upeo tofauti wa Elimu
Mlelewa anauelewa zaidi kuliko mlezi wake. Hivyo kupelekea wasiwasi kwa mlezi juu ya mlelewa wake na kumwona mtu wa majivuno. Na mlezi kujisikia inferior.

Kutofautiana kwa damu
Nikiwa na maana kwamba mlezi anamwono tofauti toka siku ya kwanza anapomwona hivyo anajenga uadui baina yake na mlelewa pasipo kuwa na sababu yoyote ya msingi.

Kadiri siku zinavyozidi kwenda na anavyozidi kumfahamu kijana ndivyo anavyozidisha uadui kwa kijana. Kwani nafasi kubwa ya mlezi ni kumwongoza kijana, na kumwonesha njia ya kupita lakini huyu ataelekea zaidi kutafuta mapungufu ya kijana. Ili aweze kumtoa.

Kuwa mlezi ni karama, au kipaji
Si kila mmoja anaweza kuwa mlezi. Wapo waliopewa dhamana hii ingawa kwa wenyewe hawana mwelekeo nayo. Lakini kwa kuwa wanataka kuonekana katika jamii na kuheshimika wanajikuta wanapokea madaraka amboyo hawayawezi, na hivyo ufanisi wake kuwa kuwa kitendawili kwao.

Mlezi kutumia zaidi sheria badala ya upendo
Wapo walezi tuliowashuhudia wakitumia sheria zaidi badala ya upendo. Kuitwa mlezi ni dhamana kubwa unayokabidhiwa kutunza Roho za watu.
Na haina maana kwamba uvimbe kichwa na kufanya unalotaka juu ya wale unaowalea. Badala yake uanatakiwa kuwa kama Mama au Baba katika kuwalea kundi ulilokabidhiwa.

Kumbuka kwamba utaitwa kutolea hesabu mbele yake yeye aliyekuumba, je utatoa hesabu ya wangapi umewafukuza au utatoa hesabu ya wangapi umefanikiw kuwafikisha kwake kadili ya mwongozo wake. Unapaswa kuwa nuru ya mwanga kwa wale unaowaongoza. Kemea panapo paswa kukemea, umpe mwanga kijana anapoelekea kupotea njia. Sifu pale kijana anapopaswa kusifiwa.


Kutokukubaliana na ukweli wa mabadiliko ya wakati
Wapo walezi ambao hawaendani na walelewa wao kutokana na ukweli kwamba wanatofautiana katika nyakati za kukua kimaisha.

Nikiwa na maana kwamba mlezi ni mtu wa mwaka 47, na mlelewa ni mtu wa karne ya 21, unategemea kwamba kutakuwa na uwiano wa mawazo kati ya hawa watu. kwani tayari mlelezi anatofauti kubwa sana na mtazamo tofauti wa mambo kuliko kijana. Hivyo kijana kutoridhika na mlezi na mlezi kutoridhika na walelewa wake.
Katika mazingira haya tegemea kuwepo kwa migongano mbali mbali na hata kuwapoteza baadhi ya vijana.


SINTA   NI  MAREHEMU JAMANI

















Niliamini kwamba wanadamu kwa kuwa na upeo wa akili tutakuwa na uwezo wa kupendana kama wanadamu lakini nimekuja kugundua kuwa anayeweza kukuangamiza ni ndugu yako wa damu au rafiki yako mpendwa. Toka hapo nikajifunza mambo yafuatayo:-
Usipende kumwamini kila mtu
Si kila unayemwomba ushauri atakupa ushauri bora
Na si kila mwenye kipara au mwenye mvi anahekima au busara.



No comments: