Monday, January 21, 2008

Tofauti baina ya Kumjua na kumfahamu mtu

Lugha yetu sasa inakuwa, ninafurahi kwamba tuna maneno yanayoweza kuelezea lugha ya Upendo wa kawaida na upendo wa kina au wa hisia. Na maneno hayo ni ' nani unamfahamu' na 'nani unamjua' kwenye kiingeleza ni sawa na maneno kama 'Love and Like'.

Haya maneno haya yanaweza kupamba sanaa ya Kiswahili na mtu akaelewa zaidi ya neno linavyojieleza, kwa maneno mengine ningeweza kusema maneno haya yanachukua pia lugha ya picha ambapo mtu unahitaji kweli kuwa na picha halisi ya jambo lenyewe unapotaka kutofautisha na lingine.

Mwanaume anauweza wa kumjua mwanamke na hawa wawili wakawa mwili mmoja kwa kubariki ndoa yao Kanisani au kwa ndoa ya mkeka. Mwanamme hanauwezo wa kumjua mwanaume mwenzake isipo kuwa anamtamfahamu tu ni kiwa na maana kwamba Mungu alitoa ruhusa ya mme kumjua mke na sio Mwanaume kumjua mwamme mwenzake hapa mambo haya endi hivi.

Mimi binafsi napinga sana Ushoga na ndoa za wanaume kwa wanaume, huu haukuwa mpango wa Mungu kumwumba mwanadamu, kama ulikuwa hivyo basi asingali uchukua ubavu wa Adamu na kumwumba mwanamke awe msaidizi wake.

Kwani ukifuatilia Biblia kitabu cha Mwanzo sura za mwanzoni tu, ambapo Mungu anazungumzia zaidi juu ya swala la uumbaji wa Mbingu utagundua kwamba ni kwa vipi wanadamu tumeingia wehu wa kuoana wanaume kwa wanaume, kitu ambacho haukuwa mpango wa Mungu.

Ni nakushauri ndungu yangu na mpendwa wangu mara nyingi sisi viongozi wenu tunawapotosha njia kwa sababu tu ya kutaka masirahi binafsi, sasa nakushauri tumia busara kufanya jambo jiulize sababu za wewe kujiunga na jambo furani.

Ukiona kunafaida basi chukua uamzi, lakini ukigundua kwamba kunahasara zaidi, hata hapo pi huna budi kuchukua uamuzi wa kuachana na njia hiyo kwa nini kujifedhehesha kwa jambo lisilo na msingi?

No comments: