Ndugu yangu mazingira yanalindwa na sisi sote si jukumu la serikali wala mgambo kulinda mazingira. Kwani ukilinda mazingira ni sawa na kuulinda uhai wako. Mazingira ni uhai, kutokana na mazingira kuwa katika hali nzuri tunapata mvua, na mvua inafaida nyingi. Tunapata maji ya kuzalishia Umeme, na pia tunatumia maji haya haya katika umwagiliaji wa mashamba na si hayo tu, tunapata maji safi kutokana na kutunzwa vyema kwa mazingira na vyanzo vyake. Je, unapokata miti unafikiria haya yote, au unatafuta faida yako binafsi, na ninyi mnaotengeneza mkaa kwa kukata miti ovyo kweli mnaharibu mazingira kwa asilimia kubwa sana, hivi mnajua au mlikimbia shule kwa sababu ya kuogopa umande? Matokeo yake ndiyo haya sasa mnashindwa kuchambua lipi la msingi na lipi linahasara kubwa kwa jamii, ndugu yangu nakushauri Elimu haina mwisho nenda kasome sasa na ujue faida za mazingira.
MILIMA YA ULUGURU KUTOKEA STENDI ZA MABASI YA HOOD HOOD MJINI MOROGORO
MTO RUAHA UNAOTENGANISHA MKOA WA MOROGORO NA IRINGA
MILIMA YA ULUGURU KUTOKEA STENDI ZA MABASI YA HOOD HOOD MJINI MOROGORO
MTO RUAHA UNAOTENGANISHA MKOA WA MOROGORO NA IRINGA
Picha kwa uhisani wa blog ya kaka Michuzi
No comments:
Post a Comment