Ingawa watu wanamwona kama kakosea na huenda ameidhalilisha Serikali, kwa upande mwingine amefanya jambo la busara sana, kujitoa katika madaraka ili mwingine ashike nafasi yake. Wengi hasa waliomadarakani huwa hawawezi kujinyenyekesha hivi, ila huyu ameweza kufanya ili kutunza heshima ya Serikali na ya viongozi wenzake. Tuige mfano wake, kwa kuweza kujishusha bila kujali kupoteza heshima zetu katika jamii. Bila Hekima hii ya kukubali kushindwa, yangetukuta ya watu wa Kenya, kuanza kuchinjana kama wanyama, sababu ni nini, jambo la kwanza ni kutokukubali mabadiliko kwa sababu ya masilahi ya Tumbo langu, na sio maisha mazuri kwa kila mtu.
pongezi
Waziri mkuu mpya mh. pinda akipongezwa na waziri mkuu aliyepita kabla yake mh. lowassa mara bada ya kuapishwa leo ikulu ndogo ya chamwino, dodoma
No comments:
Post a Comment