Wednesday, January 23, 2008

Jitahidi uwe sababu ya mwingine kuwa na furaha

Katika maisha unapaswa kuwa sababu ya furaha kwa mwingine, lakini kinyume chake wengi tumekuwa sababu ya huzuni kwa wapendwa ama marafiki zetu. Mimi binafsi nimejiuliza maswali kadhaa nikiwa na lengo la kutaka kujua kwa nini tunakuwa mara nyingi sababu ya kuwafanya watu wengine kuwa na huzuni? Nika ng'amua kwamba mara nyingi haturidhiki na mafanikio ya wenzetu na hasa pale wanapooneka kuwa na mafanikio zaidi ya sisi.
Jambo lingine ambalo nimefikia mwafaka ni kwamba, hatuchukui nafasi kuwa fahamu wapendwa wetu, ama marafiki zetu. Tunajikuta tupo nao katika mahusiano lakini sisi kwa sisi hatufahamiani kwa kina nikiwa na maana ya :-
  • Kwanza kutambua maelekeo ya mwingine
  • Na kwa wapenzi kutambua mahitaji yako na ya mwenzako
  • Kuongelea juu ya tofauti zinazojitokeza baina yetu na kuzipa suruhisho
  • Kufahamu mipaka katika mahusiano yetu na Marafiki zetu na hata wapenzi wetu
  • Jambo lingine ni kuwa na mtazamo chanya juu ya mpendwa wetu au mwandani wako
  • Kuaminiana ni jambo mhimu na katika kukuza mahusiano baina yetu
  • Na sisi tulio marafiki tuwe waaminifu wa kutunza siri za wale marafiki zetu
  • Muwe watu wa kuelezana mahitaji yenu, ungependa mpenzi akufanyie nini na wewe umfanyie nini.
  • Epukeni kulaumiana, kuuziana majungu hakukuzi mahusiano yenu zaidi ya kuwatenganisha
  • Kaeni pamoja na kuongelea maisha yenu ya baadaye mnapenda yawe ya mtindo gani
Nimekuwekeeni baadhi ya kweli zingine hapa chini ili kuwa na mwelekeo katika maisha. Jaribu kutafsiri nini maana ya maisha kwa kadiri ya mtazamo wako au kwa kadiri ya uwezo wako wa kutafsiri mambo mbali mbali unavyoyaona katika kuishi kwako, yana mana gani kwako na kwa mahusiano yako na wale uwapendao.


These are the facts of life.




FunAndFunOnly (www.mails4u.net.tc) - SridhaR

FunAndFunOnly (www.mails4u.net.tc) - SridhaR

FunAndFunOnly (www.mails4u.net.tc) - SridhaR

FunAndFunOnly (www.mails4u.net.tc) - SridhaR

Justify FullFunAndFunOnly (www.mails4u.net.tc) - SridhaR

FunAndFunOnly (www.mails4u.net.tc) - SridhaR

FunAndFunOnly (www.mails4u.net.tc) - SridhaR

FunAndFunOnly (www.mails4u.net.tc) - SridhaR

FunAndFunOnly (www.mails4u.net.tc) - SridhaR

FunAndFunOnly (www.mails4u.net.tc) - SridhaRJustify Full

FunAndFunOnly (www.mails4u.net.tc) - SridhaR



No comments: