Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 26, na niko single, naomba unipokee vile nilivyo na mfumo niliyojichagulia katika maisha. Napenda sana kusoma, Lengo ni kuwa na ufahamu mpana katika kuchambua mambo, siwezi kujua kala kitu lakini napenda nifahamu walau kitu furani. Naomba uwe huru kuchangia mawazo yako, na kukosoa pale panapohitajika kukosoa maana wengine hawafahamu maana ya kumsahisha mwingine alipokosea wanataka afanye yale ambayo wanayataka wao, sasa huko ndugu yangu nikutaka kunifanya mimi niwe wewe na kumbe haiendi hivi mimi ni mimi na wewe ni wewe, hatuwezi kufanana hata siku moja, tunaweza kuwiana ktk kufikiri. Lakini hatuwezi kulandana katika mawazo, yaani vile unavyofikiri wewe na mimi nifikiri vivyo hivyo na kwa wakati ule ule, hilo aliweza Mungu tu, na Malaika. Ndiyo maana kila mwanadamu ameumbwa peke yake hakuna wa kumfananishwa naye, tunachanganya tu mara ooh huyu anafanana na yule. Kwa nini tusiseme kuwa huyu ni yule na tunatumia neno huyu anafana na yule. Hii yote ni kumainisha kwamba hakuna anayefanana na mwingine, kwa sura au kwa tabia watu wote ni tofauti, wana wiana katika mambo machache tu. Nakutakia usomaji mwema.
No comments:
Post a Comment