Hakuna kitu kitakacho weza kufanya maisha yako kuwa ya furaha kama hutakubali kujipokea mwenyewe na kupanga mfumo mzima wa maisha yako. Wengi tunajikuta katika mahangaiko na mafarakano katika uhusiano iwe wa ndoa, au marafiki wa kawaida. Je ulisha wahi kukaa chini na kujadili kwa nini hili litokee, na je ni kweli kwamba katika haya yote hakuna jibu kwa matatizo hayo.
Mpenzi msomaji wangu katika kuchunguza hilo nimegundua kwamba tuliowengi hatuipi nafasi mioyo yetu kuchagua kile kilicho halali kwa matakwa yetu. Bali tunafuata mwelekeo wa mapendeleo yetu na tunaacha nafasi mhimu ya moyo kuupa nafasi ya kuchagua kilicho cha dhamani zaidi ya furaha ya siku moja, ambao tuliowengi tumekua tukiililia au kuionea fahari. Hapa nina maana kwamba kama mwanamke ameahidiwa kuoelewa basi atataka haja hiyo itekelezwe wakati hana uhakika wa kweli kama mpenzi wake anampenda kwa dhati.
Kunasemi zisemazo kwamba; Mwanamke anapotoa uamuzi wa kuolewa anafanya hivi akitegemea kwamba mwanamme anayeolewa naye atabadilika baada ya wao kuwa mke na mme; Pole ndugu yangu umepotea, badili mwelekeo olewa na mtu mwenye mapenzi ya dhati na ambaye yupo tayari kutoa dhamiri yake kwa ajili yako.
Na kwa upande mwingine, Mwanaume anamwoa mwanamke na kumleta ndani ya nyumba akitegema kuwa hatabadilika; Mungu wangu mwanadamu mbona unakuwa kigegeu hivi, sasa nikutendee nini ndipo ulidhike? Naamini wanawake wengi wanavumilia katika mahusiano ila wapo ambao nao ni wasumbufu, kwasababu tu ya tamaa, na wengine hujikuta wanabadilika kwa kuwa maisha magumu ndani ya ndoa, na wengine umasikini, wanataka kupata chochote au kuiga ufahali wa wengine.
Swali linakuja je, unafikiri kukamatana ugoni na kuoneshana kwenye vyombo vya habari kwamba nataka kumshikisha adabu ajifunze ni njia sahihi ya kutatu matatizo katika jamii kama watu hawata tumia njia ya kuuweka wazi moyo wao kwa kile kweli wanacho kipenda na kukitamaani?
Nimeweka baadhi ya Picha hapa zinapendeza sana lakini nichangamoto kwamba kweli tulicho kiamua pamoja na kukubaliana basi kiheshimiwe na kuthaminiwa kama kweli hunipendi sema toka mwanzo liwe wazi usitake maisha ya mtelemko kwa kuwa unayemwoa ananafasi nzuri na wewe unavimba kichwa kwa sifa ya kazi yake na sio mapenzi ya kweli. Wewe utakuwa msaliti.
Maisha ya ndoa nikuwa tayari kwa ajili ya mwingine wakati wa raha na shida kwa furaha na amani bila majuto.
Picha kwa hisani ya kaka Michuzi.

No comments:
Post a Comment